Friday, 17 April 2015

Habari zaidi Kuhusu Watu 9 Waliokamatwa Msikitini na Silaha, Milipuko, Majambia na Bendera ya Al Shaabab Morogoro

 

Jeshi la polisi mkoani Morogoro limekamata watu 9 wakiwa na silaha za kulipua na nguo za jeshi la wananchi wakiwa wamejifungia katika msikiti wa Suni Kidatu wilayani Kilombero mkoani Morogoro.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amesema tukio la kukamatwa kwa watu hao limekuja kufuatia jeshi la polisi kupata taarifa za uhalifu ambapo jambazi mmoja aliruka katika bajaji na kisha kumjeruhi askari shingoni ambapo wananchi wenye hasira kali walioshuhudia tukio hilo walimkimbiza jambazi huyo akiwa na silaha na kisha kumchoma .
Kamanda Paul amesema kufuatia tukio hilo jeshi la polisi liliongeza nguvu ya askari ambapo walifanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wengine wakiwa katika msikiti wa Suni Kidatu na baada ya kupekuliwa wamekutwa na vifaa vya milipuko nguo za kijeshi la wananchi wanaendelea kuwashikilia watuhumiwa na kuna taarifa kuwa watuhumiwa hao walijiandaa kufanya tukio la uhalifu .
Aidha kamanda paul amewashukuru wananchi wa ruhembe kidatu wilayani kilomeroa mbao wametoa ushikiano kufanikisha kukamtw akwa watuhumiwa hao.

Wednesday, 3 December 2014

MAHAFALI YA TISA YA AJTC YAFANA!!!

Wahitimu wa chuo cha uandishi wa Habari na utangazaji Arusha wakiingia ukumbini kuhudhuria sherehe za mahafalinya tisa yaliyofanyika katika ukumbi wa PPS uliopo JR mbauda jijini Arusha

wahitimu hao wakiimba wimbo wa Taifa la Tanzania

baadhi ya wakufunzi wakimsikiliza mgeni rasmi akiwaasa wahitimu kuzingatia maadili ya uandishi wa habari  katika mahafali hayo
Mgeni Rasmi katika mahafali hayo Bwana meneja wa kituo cha radio Triple A cha jijini Arusha

Baadhi ya wafanyakazi wa Ajtc waliohudhuria katika mahafali hayo wakimsikiliza mgeni rasmi alipokuwa akihutubia katika mahafali hayo

MADAM Neema Mwaipela akiwakaribisha  wageni waalikwa katika mahafali hayo

wahitimu hao wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi

Emmanuel Ndanshau ambaye alijinyakulia tuzo ya kiongozi bora katika mahafali hayo akimsikiliza kwa makini mgeni rasmi

Makamu mkuu wa chuO ELIFURAHA SAMBOTO kushoto akimkabidhi tuzo mgeni rasmi mwenye joho jekundu ambaye ni  meneja wa triple A fm ya jijini Arusha

MAHAFALI YA AJTC YAFANA